Kuhusu Sisi
Umoja wa Watendaji Tanzania
Bi. Victoria Malindila
MwenyekitiHISTORIA
Historia ya Watendaji nchini Tanzania imejengwa juu ya msingi wa kusimamia miradi ya maendeleo, miundombinu,ustawi wa jamii,kutafasiri na kusimamia utekelezaji wa sheria, Ulinzi na Amani katika ngazi za utawala. Tangu baada ya uhuru wa Tanzania mwaka 1961, Watendaji wamekuwa mhimili muhimu katika utekelezaji wa sera za Nchi,ukusanyaji wa mapato,taarifa za maendeleo,usimamizi wa miradi ya kijamii pamoja na kuhakikisha huduma za msingi zinawafikia wananchi.
Umoja wa Watendaji Tanzania (UWATA) una dhamira ya kuimarisha mshikamano,taaluma,uwajibikaji na maendeleo ya Watendaji Nchini.